12 Machi 2020 - 07:25
Answarullah: Marekani ndio mhusika mkuu wa mauaji na mzingiro dhidi ya Wayemen

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen ameitaja Marekani kuwa muhusika mkuu wa mauaji na mzingiro dhidi ya watu wa Yemen.

(ABNA24.com) Mohammed Ali al-Houthi ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo ameandika kuwa, raia wa Yemen wanauawa na kuzingirwa kwa silaha za Marekani. Al-Houthi ameongeza kwamba, misada ya Marekani kwa wavamizi wa Saudia, ni hatua ya kichokozi na ya jinai kubwa.

Hii ni katika hali ambayo Mujtahid, mwanaharakati na mfichuaji mashuhuri wa habari za ndani ya Saudia ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, jumla ya askari 110 wa Kimarekani wamepiga kambi katika pwani ya Balhaf, ya mkoa wa Shabwah nchini Yemen wakiwa na helikopta 10 za Apache, magari 10 ya deraya na ngao 4 za makombora za Patriot.

Kadhalika Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen, Mohammed Ali al-Houthi amesema kuwa muungano vamizi wa Saudia na Marekani unahusika katika kuchafua maji ya Yemen na kubainisha kwamba, kile kinachotokea katika mikoa ya pwani ya kusini ya nchi hiyo ya Kiarabu kukiwemo kushuhudiwa mada za kemikali na kibiolojia ndani ya maji ni matokeo ya kuwasili meli za Marekani katika maji ya eneo hilo.

Katika uwanja huo, Muhammad Abbad al-Faqih, Mkuu wa Usimamizi wa Uvuvi nchini Yemen amesema kushuhudiwa samaki waliokufa katika pwani ya Aden, ni ishara ya kuchafuliwa maji.

...........
340